Msaada wa kujijenga baada ya COVID-19?

Tala imeanzisha Msaada wa kujijenga baada ya COVID-19 ili kusaidia wakenya kukabiliana, kujiinua na kujirejesha kutokana na janga la virus vya Corona. Juu ya hayo yote msaada huu utatoa Mikopo ya Kusaidia Jamiii kwa ajili ya biashara muhimu. Kwa, habari za kuaminika kuhusu COVID-19 na mengine kuhusu msaada huu, tembelea: https://tala.co.ke/covid-19-resources/

Mkopo wa Kusaidia Jamii ni nini?

Mkopo wa Kusaidia Jamii ni mkopo uliozinduliwa na Tala kama mojawapo wa juhudi za kusaidia jamii za Kenya wakati wa janga la COVID-19. Wateja wa Tala wanaofanya biashara zenye umuhimu kwa jamii yao wanaweza kutuma maombi ya Mkopo wa Kusaidia Jamii wenye masharti maalum.

Unafanyaje maombi ya Mkopo wa Kusaidia Jamii?

Wateja wanaohitimu wanaweza kuomba kwenye app ya Tala.

Nani anayehitimu kupata mkopo huu?

  • Wafanyibiashara wote wanaopeana huduma muhimu kwa jamii yao wanahitimu kuomba.
  • Wafanyibiashara lazima wawe bado wanaweza kuhudumia jamii zao kwa namna fulani wakati ambao biashara zimefungwa juu ya janga la COVID-19.

Unafafanuaje “biashara muhimu”?

Biashara muhimu zinafafanuliwa kama biashara zinazopeana huduma za kiafya, chakula na maji, vifaa muhimu vya nyumbani, elimu, na vifaa vinavyohusiana na huduma zilizotajwa.

Mkopo utatumwa lini?

Waombaji watakaguliwa kila wakati na kuarifiwa kuhusu uamuzi wa Tala ndani ya wiki mbili baada ya kukamilisha maombi yao.Mara tu ukichaguliwa, Tala itawasiliana nawe kupitia simu na mikopo itatumwa ndani ya masaa 24. Utaarifiwa mara tu uamuzi utakapofanywa.

Last updated:
Was this article helpful?
1057 out of 1293 found this helpful