Nini kitafanyika nikichelewa kulipa ama nikilipa mapema?

Kulipia kabla

Hakuna malipo ya kuchelewa (late fee) kutokana na kulipa mapema. Kwa kweli, kulipa mapema na kwa wakati kutakusaidia kuhitimu mikopo mikubwa kiasi baadae!

 

Kuchelewesha Malipo

Ni muhimu kufanya malipo yako kwa wakati ili kuweza kuendelea kufaidika kwa mikopo ya Tala, ya haraka na yenye riba ya chini. Kukosa kulipa mkopo inaweza kusababisha malipo ya kuchelewa (late fee), kiwango cha mkopo kilichopungua, na hata kukosa kupata mikopo kutoka kwa wakopeshaji wengine.

 

Kukosa Kulipa

Unaweza kupigiwa simu na wahudumu wetu wa makusanyo usipolipa mkopo wako kwa wakati. Ikiwa utakaa kwa muda mrefu bila kulipa, unaweza kufungiwa kutumia Tala na pia kuripotiwa kwenye CRB.

Last updated:
Was this article helpful?
412 out of 468 found this helpful